MPENZI BORA.
Picha: Hisani ya Dreamtimes.com Sikia mpenzi sikia, ewe wangu wa ubani Wewe ndiwe malkia, nikuenziye moyoni Habibi nakusifia, wangu namba wani Nakupenda wangu muhibu, mwingine sitamani. Usojua kukasirika, vipodozi wala kupara Mwenziyo nachacharika, unipigapo mikwara Umeniteka hakika, nakughania mikarara Nakupenda wangu muhibu, mwingine sitamani. Mama huna maringo, wala pesa kutakia Kifua chako mviringo, lazizi wanivutia Halafu yako shingo, tisti imesimamia Nakupenda wangu muhibu, mwingine sitamani. Siwatamani kabisa, warembo wa humu mjini Naogopa watanitosa, huwapati mapenzini Punde pesa nikikosa, watatoroka nyumbani Nakupenda wangu muhibu, mwingine sitamani. Kipi sikipati kwako, mwendani wangu wa dhati Mtima mehamia kwako, nikande kama chapati Niamini mimi wako, moyo unapuma ati Nakupenda wangu muhibu, mwingine sitamani. Kwanza huo wako mwanya, mwenzio najiishia Unazo fikira chanya, wanipa...