MPENZI BORA.

    Picha: Hisani ya Dreamtimes.com

Sikia mpenzi sikia, ewe wangu wa ubani
Wewe ndiwe malkia,  nikuenziye moyoni
Habibi nakusifia,  wangu namba wani
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Usojua kukasirika,  vipodozi wala kupara
Mwenziyo nachacharika,  unipigapo mikwara
Umeniteka hakika,  nakughania mikarara
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Mama huna maringo,  wala pesa kutakia
Kifua chako mviringo,  lazizi wanivutia
Halafu yako shingo,  tisti imesimamia
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Siwatamani kabisa, warembo wa humu mjini
Naogopa watanitosa, huwapati mapenzini
Punde pesa nikikosa, watatoroka nyumbani
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Kipi sikipati kwako, mwendani wangu wa dhati
Mtima mehamia kwako, nikande kama chapati
Niamini mimi wako,  moyo unapuma ati
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Kwanza huo wako mwanya, mwenzio najiishia
Unazo fikira chanya, wanipandisha hisia
Utakacho nitafanya, kwangu uzidi bakia
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Njoo uishi na kwangu,  pekee yangu siwezi
Uupoze mtima wangu,  majeraha yote mjuzi
Milele ubaki wangu, usinikimbie kipenzi
Nakupenda wangu muhibu,  mwingine sitamani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NIKUSAMEHE UKAE WAPI?